MAMBO YA MJINI HAYA:
HII kali!
Jamaa mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, alikutwa
amelazwa chini akiwa amelewa chapachapa, maeneo ya Mtaa wa Kongo,
Kariakoo jijini Dar, huku kawekewa karatasi kifuani na wahuni ikisomeka;
“for sale” (anauzwa).
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mwenzake huyo baada ya
kuona swaiba wake hajitambui, aliamua kumshusha maeneo hayo na kumlaza
chini kisha kumuwekea karatasi kifuani iliyokuwa na maandishi
yaliyosomeka; “for sale”.Chanzo kiliendelea kuweka wazi kuwa mtu huyo
alianza kuwaambia watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo kuwa kama
kuna mtu ana shida na ‘mtoto’ anapatikana kwa bei ya maelewano huku
akiwakataza kumpepea.
Mapaparazi wetu walifika eneo la tukio na kujionea baadhi ya vijana
wa mjini wakitaka kumfanyia kitu mbaya lakini kuna mzee mmoja aliwazuia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni