Mratibu
wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima (kushoto) akitoa maelezo ya
kikundi cha kina mama ambao ni walengwa wa mradi wa Ukimwi unaofadhiliwa
na SIDA chini ya shirika la kazi duniani (ILO), kwa Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, katika ziara ya kikazi
ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa
mkoani Iringa na Njombe. Kulia ni Practice Specialist HIV/AIDS, Dr Bwijo
Bwijo.
Na Mwandishi wetu, Iringa
KIKUNDI
cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba,kilichopo Wilaya ya Iringa,
wameomba kusaidiwa vifaa vya kisasa vya ufinyanzi, ili waweze
kutengeneza vitu bora vitakavyokubalika katika soko.
Maombi
hayo wameyatoa katika risala yao kwa Mratibu wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa UNDP, Alvaro Rodriguez.
Mratibu
huyo alikuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa
na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.
Makundi
yaliyotembelea ni yale ya ujasiriamali, yanayosimamiwa na Shirika la
Kazi Duniani (ILO) chini ya mpango wa Kupunguza Maambukizi ya UKIMWI kwa
Njia ya Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wafanyakazi walio katika Sekta Isiyo
Rasmi kando kando mwa Barabara Kuu iendayo Tanzania-Zambia maarufu kama
“Corridor Economic Empowerment Project (CEEP) “
Aidha
makundi mengine yaliyotembelewa ni ya wakulima wanaosaidiwa pembejeo na
wanaotengeneza vikapu na kufanya shughuli binafsi ikiwamo mabucha.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa
amembeba mtoto wa mwanachama wa Mtwango SACCOS ya wilaya ya Njombe.
Mmoja
wa wanachama hao Anna Nyongole alisema wanafanya kazi hiyo katika
mazingira magumu, kwani bado wanatumia mikono pekee, badala ya kutumia
vifaa vya kisasa, na hivyo kusababisha bidhaa zao kukosa ushindani
katika soko jambo linalowadumaza kiuchumi.
“Tunatengeneza
vyungu, sufuria, majiko, mitungi ya maji na ya maua, na vitu
mbalimbali, lakini changamoto yetu kubwa ni namna tunavyotengeneza,
kwani hatuna mashine za kutengenezea vitu hivyo wala mitambo ya
kuchomea, tunaiomba serikali na wadau wa maendeleo nchini watusaidie,
kwani tukipata vifaa vya kisasa tutaweza kutengeneza vitu vingi kwa muda
mchache kuliko ilivyo sasa,” alisema Nyongole.
Naye
Zena Omary amesema kukosekana kwa usafiri wa gari kwenda kusomba
udongo wa kufanyia ufinyanzi kunawafanya kutembea umbali wa kilomita 40
kwenda na kurudi, kutoka katika eneo la Ikekeke katika kijiji cha
Kitelewasi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika
picha ya pamoja na Wanchama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo
kinachofadhiliwa na SIDA chini ya Shirika la kazi Duniani (ILO).
“Tunakokwenda
kuchimba udongo ni Ikekeke katika kijiji cha Kitelewasi, tunatembea
kilomita 20 kwenda na kurudi kilomita 20, kwa hiyo unajikuta siku moja
umeshindia kuchimba udongo na kusomba tu, na kwa kuwa tunajitwisha
kichwani, huwezi kuchukua udongo mwingi,” alisema Zena.
Licha
ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, akinamama hao wamesema kupitia
mafunzo ya UKIMWI na Ujasiriamali waliyopata kutoka ILO wameweza
kuboresha biashara hiyo ya ufinyanzi kwa kujenga banda la kuhifadhia
bidhaa hizo, kuweka akiba na kukopeshana katika kikundi hatimaye
wamefanikiwa kuyabadili maisha yao kwa kujenga nyumba bora na hata
kuwasomesha watoto wao kwa kumudu gharama za ada.
“Hapa
kila mmoja wetu anayo nyumba ya kisasa ya tofali za kuchomwa na
iliyoezekwa kwa bati, na pia tumefanikiwa kusogeza huduma ya maji ya
bomba katika nyumba zetu, ili kupunguza usumbufu wa kuchota maji
visimani... kwa kweli biashara hii ya ufinyanzi imetusaidia lakini
tukiboreshewa zaidi mazingira tutakua zaidi kiuchumi,” Walisema.
Msafara wa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro
Rodriguez ukiongozwa na Mratibu wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima
(kushoto) kuelekea kukagua baadhi ya miradi inayofadhiliwa na mashirika
ya Umoja wa Mataifa wilayani Njombe.
Hata
hivyo Umoja wa Mataifa UN kupitia Shirika la Kazi Duniani “ILO” Kwa
mkoa wa Iringa pekee- limefanikiwa kuwafikia akinamama na vijana wapatao
1,000 wa vikundi mbalimbali vya kiuchumi na vyama vya Kuweka na Kukopa
(SACCOS), huku wanachama wa vikundi hivyo wakipatiwa mikopo, Elimu ya
Maambukizi Virusi vya UKIMWI, pamoja na mafunzo ya Ujasiriamali.
Mratibu
huyo alitembelea vikundi hivyo kuona namna msaada wa Umoja wa Mataifa
ulivyobadili maisha ya wahusika ambao walikuwa katika mazingira magumu
hapo awali.
Makundi
mengine yaliyotembelewa yapo Nyololo na pia hospitali ya Mafinga
ambako kuna mafunzo yanayoendeshwa kwa ajili ya ushauri nasaha kwa
wanawake wenye kuishi na VVU.
Miradi hiyo ambayo mashirika ya UNICEF na IFAD yanashiriki, imelenga
kusaidia makundi hata yale yenye wanachama wanaoishi na virusi vya
ukimwi kujitambua na kuishi kwa kujitegemea.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye
picha ya pamoja na kikundi cha kinamama wa Nyololo wanaotengeneza
vikapu.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza
na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Nyololo Centre ambao wengine
wakiwa ni ndugu wa wakinamama wanaosaidiwa na ILO.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua
shamba la Mradi wa miche na matunda ambalo linasimamiwa na wanawake wa
kikundi cha Nyololo wanaofadhiliwa SIDA chini ya shirika la kazi duniani
(ILO).
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki
kupanda mti kwenye shamba hilo kama kumbukumbu wakati wa ziara yake ya
kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani
Iringa na Njombe.
Katibu
wa Kikundi cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba, Bi. Leokadius Mfukwe
akisoma risala ya kikundi chao na changamoto zinazowakabili mbele ya
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye
miwani) alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi
inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.
Baadhi ya vyungu vinavyotengenezwa na kikundi hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni