Uchaguzi wa serikali za mitaa huko Geita umefunguliwa kwa vurugu
kubwa ambapo mkurugenzi wa siasa na uenezi wa chama cha
wananchi(CUF)katika kata ya Kagu wilayani Geita Fransisco
Kadimu(34)amenusurika kufa baada ya kukatwa mapanga kichwani na vidoleni
na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Kutokana na hali hiyo wananchi wa eneo hilo walikasirishwa na kitendo
hicho na kulazimika kupiga yowe kujikusanya na baadaye waliamua kuvamia
makazi ya watuhumiwa kisha kuyasambaza na kuchoma moto moja ya pool
table ya mtuhumiwa wa ukataji mapanga.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Desemba 14 saa 5 usiku katika
kijiji cha Kinaki kata ya Nyawilimilwa Wilayani Geita Katika mkoa wa
Geita.
Akizungumza kwa taabu na Dunia Kiganjani Blog akiwa katika hospitali
ya Wilaya ya Geita Kadimu alidai kuwa alikumbana na wakataji hao wakati
akitokea kwa katibu wa chama chake anayeishi kijijini hapo.
Alisema,akiwa ameivuka senta ndogo ya Calfonia ndipo alipokutana na
watu hao ambao aliwatambua kwa majina na sura ambao bila huruma walianza
kumkat akata mapanga kichwani na mikononi sambamba na kumpiga kwa fimbo
na marungu hali iliyopelekea kupoteza fahamu.
Alisema,alikuja kupata fahamu baadaye na kujikuta amezungukwa na
wananchi waliofika eneo hilo kufuatia mayowe aliyopiga kabla ya kuzirai
na ndipo walipomkimbiza katika hospitali ya Wilaya ya Geita anakoendelea
na matibabu.
Katika tukio hilo mbali na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za
kichwani pia kidole chake kimoja cha mkono wa kulia kilinyofolewa kwa
panga na kubakia na ulemavu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji cha
Nyawilimilwa Charles Kidingi alisema,baada ya tukio hilo wananchi
walihamasishana na kwenda kuvunja makazi ya watuhumiwa hao pamoja na
kuteketeza kwa moto pooltable la mmoja wa watuhumiwa hao.
Aliwataja watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo ambao ni makada wa
CCM kijijini hapo kuwa ni pamoja na Mashiku Ndezu,Deo Ndezu,na wengine
waliofahamika kwa jina moja la Raulian na Alex ambao wamekimbilia
kusikojulikana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni