Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Tanzania, Peter Jiang(Kushoto) na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Arusha, Profesa Lughano
Kusiluka, wakisaini mkataba wa Shilingi Milioni 51 kama msaada wa
kuchangia utafiti wa matatizo mbalimbali ya jamii nchini zilizotolewa na
Kampuni hiyo mwishoni mwa wiki.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Tanzania, Peter Jiang(Kushoto)
akimkabidhi mkataba, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha
Arusha, Profesa Lughano Kusiluka mara baada ya kusainishana wa Shilingi
Milioni 51 kama msaada wa kuchangia utafiti wa matatizo mbalimbali ya
jamii nchini zilizotolewa na Kampuni ya HUAWEI mwishoni mwa wiki.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Tanzania, Peter Jiang (Kushoto) na Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Arusha, Profesa Lughano
Kusiluka, wakiteta jambo mara baada ya kusainishana mkataba wa Shilingi
Milioni 51 kama msaada wa kuchangia utafiti wa matatizo mbalimbali ya
jamii nchini zilizotolewa na Kampuni ya HUAWEI Nchini mwishoni mwa wiki.
CHUO
Kikuu Cha Nelson Mandela Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) kimesaini
makubaliano ya kiasi dola za kimarekani 30,000 sawa na kiasi cha
shilingi hamsini na moja milioni kutoka kampuni ya Huawei Tanzania ikiwa
ni katika malengo mahususi ya kuwasaidia wanafunzi wa shahada ya
uzamili katika kufanya tafiti kwenye Nyanja za teknolojia na habari
(TEKNOHAMA).
Akizungumza
wakati wa kusaini makubaliano hayo jijini Arusha mwishoni mwa wiki,
Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Lughano Kusiluka amesema kuwa huu ni mwaka
wa pili wa makubaliano na Huawei ya kukisaidia chuo kiasi cha dola
30,000 kila mwaka kwa muda wa miaka mitatu katika mikakati ya kuwainua
wanafunzi wa Teknohama kwenye tafiti.
Profesa
Kusiluka aliongezea kuwa msaada huo siyo tu utakisaidia chuo na
wanafunzi kuweza kuisadia nchi yetu ya Tanzania katika kupiga hatua za
kiuchumi na maendeleo kupitia sekta ya mawasiliano na habari.
“Kama
mliovyomsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia
wahitimu, amesisitiza kuwa tafiti za kisayansi ni muhimu sana katika
kukuza uchumi wa taifa lolote lile Duniani, hivyo msaada huu kutoka
Huawei utaleta chachu kubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema
Aliongezea: “Kwa niaba ya Uongozi wa Chuo, tunaishukuru sana kampuni ya
Huawei Tanzania kwa mchango wake ambao kwa kiasi kikubwa umefanikisha
sana matokeo ya wahitimu hawa tulio nao leo.
Huawei
wamejitolea kuchangia utafiti kwa miaka mitatu na huu ni mwaka wa pili,
tunawaomba waendelee kuwa nasi hata baada ya mwaka wa tatu wa
makubaliano”
Akizungumza
kwa niaba ya wanavyuo wenzake waliofaidika, Michael Mollel alisema:
“Binafsi natoa shukrani zangu za dhati kwa Huawei Tanzania kwa mchango
huu, mimi nilifanya utafiti wangu katika jiji la Dar es Salaam,
ilinichukua miezi mitatu kukamilika, na kwa gharama zilivyo katika jiji
hilo, nimgekuwa katika hali ngumu sana na hata kushindwa kumaliza
utafiti kama siyo kwa msaada kutoka Huawei” Mollel aliongezea kuwa
mafanikio yake hadi kufikia kutunukiwa shahada ya uzamili yamechangiwa
kwa kiasi kikubwa na msaada huo wa Huawei waliotoa katika chuo cha
NM-AIST.
Kampuni
ya Huawei Tanzania mwishoni mwa wiki ilishuhudia mafanikio makubwa ya
mpango wake wa kuchangia utafiti kwa wanachuo wa shahada ya uzamili
katika Taasisi ya Sayansi na Technolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ya
Jijini Arusha.
NM-AIST
imefanya mahafali yake ya pili ambapo wahitimu wa shahada ya Uzamili
walikuwa 93 na uzamivu walikuwa 13, ambayo ni asilimia 95 na karibu
asilimia 50 ya jumla ya wadahiliwa wa makundi haya.
Wahitimu
wa shahada ya uzamili wa kike ni asilimia 33 na wa shahada ya uzamivu
ni asilimia 25. Mahafali hayo yalihudhuliwa na Rais Jakaya Kikwete,
Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal pamoja na waziri wa Sayansi na
Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.Kwa
wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo
lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp
namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni