Quick
Rocka amekanusha kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu,
Kajala Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Quick amesema ana
girlfriend hivyo uvumi huo unaweza ukamharibia uhusiano wake.“Nasema
hapana Kajala mimi sister yangu, tunafanya naye kazi na nimeunganishwa
na Lamata. Lamata ni director ninayemmfahamu zamani kidogo kipindi kile
tunafanya ‘Mbwa Mwitu’ tulikuwa wote, Lamatah, Hemedy! Unajua
mnavyofanya movie ni tofauti na kufanya video, kwa mfano wakati
tunafanya ile movie ya Wolper, tulikaa Magomeni kambini ili kujenga
chemistry. Unajua mnapoigiza kuna vitu lazima viendane. Sisi ni kambi
moja inabidi mchongo tuufanikishe,” alisema rapper huyo. “I have a
girlfriend, anavyosikia hivi vitu mimi kwa upande mmoja inaniharibia na
sijui yeye pia ana mtu wake huko kwahiyo tuna wazazi, tuna watu wetu wa
karibu ambao wanatuangalia, watu ambao wametupenda na wametuamini hivyo
halafu wakija kusikia mambo haya kwenye media wataona kumbe huwa
hamfanyi kazi, wao wanachukulia serious. Sio vitu vya kweli.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni