Watu
wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na wananchi
wenye hasira baada ya jaribio lao la kutaka kupora fedha zaidi ya
shilingi milioni 100.Watu wawili kati ya wanne wanaosadikiwa kuwa
majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya jaribio lao la
kutaka kupora fedha zaidi ya shilingi milioni 100 katika kiwanda cha
kutengeneza chokaa cha Nelkanth kilichopo eneo la Amboni jijini Tanga
kushindikana.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoani Tanga kamishina msaidizi wa polisi Juma Ndaki
amewataja majambazi waliouawa kuwa ni Timoth Charles mkazi wa Mkwajuni
jijini Dar es Salaam na mwinyimkuu Hamisi mkazi wa mtaa wa chanika ambao
walikuwa wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya boxer huku wenzao wawili
wakikimbia kusikojulikana.
Wakielezea
vyema tukio hilo baadhi ya wafanyakazi na walinzi wa kiwanda hicho
wamesema majambazi hao baada ya kuingia ndani ya geti la kiwanda hicho
walikwenda moja kwa moja katika chumba cha mhasibu na walipofika
walianza kunyonga mhasibu lakini wakati wa kujitetea ndipo sekretari wa
mhasibu alipotoka nje na kupiga mayowe kuashiria bosi wake amevamiwa na
majambazi.
Kufuatia
hatua hiyo mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho Bwana Amiry
Ramadhani ameliomba jeshi la polisi mkoani Tanga kuhakikisha wanafanya
upelelezi wa kutosha ili kujua kama huenda kuna baadhi ya wafanyakazi
ambao wamekuwa chanzo cha tukio hilo.Chanzo EATV.TV
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni