Jumatano, 10 Desemba 2014

Katibu wa CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA ameahidiwa ushindi



 Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA akiwahutubia wananchi wa kijiji cha kihesa mgagao.

 baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano huo.


NA FREDY MGUNDA,KILOLO
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringaha HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika kijiji cha kihesa mgagao na kulakiwa na mamia ya wananchi katika kijiji chicho kilichpo wilayani kilolo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni hizo Katika Kijiji hicho  HASSANI MTENGA alisema kuwa kampeni hizo zinazotaraji kufikia kikomo Disemba 13 Mwaka huu, zilipaswa kufanyika muda mrefu hivyo kilichochelewesha uchaguzi huo ni mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.
MTENGA ametumia nafasi hiyo pia kuwanadi mgombea nafasi ya uenyeviti wa kijij hicho ambapo amewaomba  wananchi wa kijiji hiocho kumchagua PHILIPO KAGINE  awe mwenyekiti wao.
Akizungumzia sakata la vyama vya upinzani kutaka kugomea uchaguzi amesema kuwa wasimamizi wa uchaguzi nchini wanaangalia vigezo vya wagombea hivyo kama hawakuwa na vigezo kusingekuwa na usamaria mwema kwenye kwenye jambo.

nao wananchi wa kijiji hicho walimwambia katibu huyu kuwa mgombea wao kupitia chama cha mapinnduzi atashinda kwa kishindo kwa kuwa kijiji hicho ni ngome ya CCM.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa