MULEBA.
Matokeo ya
awali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana Desemba 14,2014, nchini
kote, yanaonesha kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kinaongoza katika wilaya ya
Muleba Mkoani Kagera kwa kupata viti 52 huku CHADEMA kikiwa na viti 32 katika
ya vito 166 vinavyowaniwa.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba ,Bw Josephat Mkude amesema matokeo hayo
yanakifanya Chama cha Mapinduzi kiwe na viti 65 baada ya kupata Wenyeviti 13
waliopita bila kupingwa wakati wa kura za maoni.
Bw Mkude amesema
wilaya ina vitongoji 752 na kwamba ukusanyaji wa matokeo unakwenda taratibu
ambapo amesema kufikia leo Desemba 15,2014, majira ya Saa 12 jioni zitakuwa
zimepatikana takwimu nyingine za matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika kwa amani
na utulivu.
Hata hivyo
Msemaji wa kambi ya upinzani kupitia Ukawa Bw Hamis Yusuf ambaye ni Katibu wa Chadema
wilayani humo amesema wamekosa ushindi katika uchaguzi huo kwa kuwa sera ya Ukawa
haikueleweka kwa wagombea wao.
BUHIGWE.
Halmashauri
ya wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imepokea matokeo ya vijiji 16 ikiwa ni
sehemu ya Matokeo ya awali ya uchaguzi katika wilaya hiyo
Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo Bw Simon Mumbee amesema kati ya vijiji hivyo, kwa nafasi ya
Wenyeviti wa Vijiji, Chama cha Mapinduzi kimepata viti 11, NCCR Mageuzi viti
vitatu wakati Chadema na CUF kila chama kimepeata kiti kimoja.
Amesema
katika nafasi za wenyeviti wa Vitongoji, CCM kimepata viti 43, NCCR na Chadema
vimepata viti 10 kila chama huku Chama cha Wananchi CUF kikipata viti vitatu.
Bw Mumbee
amesema kwa upande wajumbe wa Halmashauri za Vijiji, CCM kimepata wajumbe 101,
NCCR Mageuzi wajumbe 18, Chadema na CUF wajumbe 16 kila chama.
Mkurugenzi
huyo wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe amesema katika nafasi za viti maalum
wajumbe Halmashauri za Vijiji CCM kimepata wajumbe 64, Chadema 12, NCCR wajumbe
6 ambapo amesema bado wanaendelea kupokea matokeo ya vijiji vingine.
Akataa
kusaini: Mtaa wa
Katoma Geita Mjini wananchi wamekesha kusubiri matokeo.Mgombea wa CCM
ameshindwa na amekataa kusaini matokeo.
Mabomu
yatumika: Jeshi la
Polisi limeamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi mkoani Mwanza
katika maeneo ya Pasians, Mji Mwema, Kirumba, Ibungiro na Kitangiri baada ya
vurugu wakati wa kusubiri kutangazwa matokeo.
Kijiji
cha Muungano Kata ya Chahwa mkoani Dodoma: CHADEMA 196, ADC 38
Mbozi;
Mtaa wa Masaki:
CHADEMA 99, CCM 44
Kigoma
Mjini; Mtaa wa Gezaulole: CHADEMA 240, CCM 198
Ukonga;
Mtaa wa Kivule Majohe: CHADEMA 231, CCM 77
Musoma
Vijijini; Kijiji cha Muhoji: CHADEMA 197, CCM 464
Ubungo;
Mtaa wa Msewe:
CHADEMA 683, CCM 356
Kinondoni;
Mwenge Nzasa:
CHADEMA 344, CCM 318
Mwanga
Mtaa wa Lwami:
CHADEMA 55, CCM 35
Mererani: CHADEMA imeshinda mitaa 7 kati
ya 8
Kitongoji
cha Endulele:
CHADEMA 170, CCM 130
Monduli;
Kitongoji Kambi ya Mkaa: CHADEMA 27, CCM 13
Mwanga
Mtaa wa Lwami:
CHADEMA 55, CCM 35
Arumeru
Magharibi, Kitongoji Endulele: CHADEMA 170, CCM 130
Ushirombo
Mjini: CHADEMA
inaongoza vitongoji 10, CCM inaongoza vitongoji 4
Moshi
Manispaa, Kitongoji Longuo A: CHADEMA 206, CCM 66
Mbozi
Mtaa wa Mbugani: CHADEMA 227, CCM 160
Kata ya
Mji Mpya, Morogoro
yenye mitaa 12, CCM imeshinda mitaa 9, CHADEMA wakishinda mtaa 1 huku mitaa
miwili mpaka sasa bado vurugu zimetanda baada ya kura kudaiwa kuzidi huku watu
kadhaa wakituhumiwa kupiga kura mara mbili.
Kagondo,
Kata ya Muhutwe, Kagera: CHADEMA imeshinda mitaa 4 kati ya 5
Kufungwa
Vituo: Katika maeneo
mengi vituo vya upigaji kura tayari vimefungwa huku wananchi wakisubiri kwa
hamu kujua matokeo.
Uchaguzi
Migombani: Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa eneo la Migombani, Segerea jijini Dar umeingia dosari
baada ya Afisa Mtendaji Kata ya Segerea kutangaza kusitisha uchaguzi huo
kimyakimya bila sababu za msingi ambapo wananchi waliamua kumweka mtu kati
mpaka akaruhusu uchaguzi huo kuendelea kwa maandishi.
Akijitetea afisa huyo
alidai kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala
kufanya hivyo.
Mazimbu,
Morogoro: Eneo la
Mazimbu, Moro kimenuka mpaka wanajeshi wamelazimika kuingilia kati kutuliza
ghasia wakati wa zoezi la upigaji kura.
Kawe,
Dar: Uchaguzi
wadaiwa kuingia dosari baada ya mgombea wa CCM kutoa amri ya vitabu kufungwa
kabla ya muda ulipangwa.
Kigogo,
Dar: Mgogoro umezuka
katika Kituo cha uchaguzi Kigogo jijini Dar baada ya wananchi kudai kuwa baadhi
ya watu wamepelekwa kama mamluki eneo hilo kwa ajili ya kugipa kura.
Sokoine-Kibaoni,
Morogoro: Wananchi
eneo la Sokoine-Kibaoni, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mpaka sasa bado hawajaanza
kupiga kura mbali na wengi wao kujitokeza huku wengine wakiwa wamekodi magari
kutoka Bwawa la Kihonda umbali wa kilomita 20 kwenda kupiga kura lakini mpaka
sasa bado hawajapiga kura.
Amana,
Ilala: Baadhi ya
wananchi wameamua kususia zoezi la upigaji kura katika Kituo cha Amana, Ilala
jijini Dar baada ya mgombea Uenyekiti wa Mtaa wa Amama aitwaye Mathias Ijumba
kuondolewa katika uchaguzi dakika za mwisho kwa kile kinachodaiwa kuwa si mkazi
wa eneo hilo lakini jambo la ajabu jina like liko katika orodha ya watu
waliojiandikisha kupiga kura na mgombea huyo ameruhusiwa kupiga kura yake.
Baadhi ya
wananchi wa eneo hilo wamedai jamaa huyo anakubalika sana na huenda ndiyo
chanzo cha jina lake kuondolewa.
Dar es
Salaam: Wananchi
katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanalalamikia utaratibu wa majina
unaotumika katika zoezi la upigaji kura linaloendelea, wengi wadai kupata tabu
kuona majina yao huku wengine majina yao yakiwa hayapo kabisa katika vituo.
Shariff
Shamba, Ilala: Eneo
la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo
baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki
vimeafikiana.
Kagunga,
Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la
Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata
kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa
vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao.
Hata hivyo
Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.
Chanzo:-Radio Kwizera/Blog za Jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni