Hali ya
sintofahamu imeibuka katika mtaa wa Azimio, kata ya Kihonda katika
manispaa ya Morogoro, baada ya mwanamke mmoja, Veronica Madebe, kukutwa
akitaka kumtumbukiza mwanaye wa kiume ambaye ni pacha, mwenye umri wa
kati ya miaka mitano hadi saba kwenye kisima cha maji, kutokana na
kinachosadikiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Tukio hilo limejiri katika eneo hilo la Azimio, baada ya mwanamke
huyo kukutwa na mmiliki wa nyumba kilipo kisima hicho, Dani Haji,
akijaribu kumtumbukiza kisimani mmoja wa watoto wake pacha, kwa madai
yaliyoelezwa huenda ni kupungukiwa akili, ama ni imani za kishirikina.
Amedai kutumwa na wakazi wawili wa eneo hilo kufanya hivyo, na wakati
mwingine kudai alikuwa kwenye kifungo na alipaswa kutoa kafara ya mtoto
wake kwa kumtupa kisimani ili afunguke baada ya kuokoka kiimani, jambo
lililothibitishwa pia na mmoja wa wajumbe wa serikali za mitaa katika
eneo hilo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni