Maafisa
wa utawala nchini Indiaa wanafanya uchunguzi kufuatia madai ya wagonjwa
15 kupofuka baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutibu ugonjwa ujulikanao
kama ''mtoto wa Macho' au Cataract bila malipo.
Upasuaji huo ulikuwa unafanywa na shirika moja lisilo la kiserikali katika kambi iliyotengewa matibabu hayo.
Maafisa
wakuu wanasema kua kambi ambako upausuaji huo ulifanyika haikuwa na
idhini inayostahili na pia waliokua wanaufanya upasuaji huo hawakuwa na
vifaa vinavyostahili.
Lakini tajiri mmoja ambaye alifadhili mradhi huo, alisema wagonjwa wote 49 wa macho waliofanyiwa upasuaji walipewa huduma nzuri.
Mfumo
wa afya nchini India uko chini ya darubini hasa baada ya wanawake 15
kufariki baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufungwa kizazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni