Mwaandishi wa Mmarekani, Luke Somers
na mwalimu raia wa Afrika Kusini, Pierre Korkie wameuwawa na
wapiganaji
wa Al-Qaeda nchini Yemen katika juhudi za kuwaokoa.Oparesheni hiyo ya kuwaokoa iliongozwa na vikosi maaulum vya Marekani na Yemen katika jimbo la kusini la Shabwa.
Mwalimu raia wa Afrika Kusini Pierre Korkie (kulia).
Rais wa Marekani Barack Obama amelaani mauaji ya kinyama ya mateka hao wawili.Walikua wanazuiliwa na wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda katika Bara arabu ambalo Marekani inalichukulia kuwa mojawapo wa matawi hatari duniani ya kundi kuu la al-Qaeda.
Shirika ambalo mwalimu huyo raia wa Afrika Kusini Pierre Korkie alikuwa akilifanyia kazi lilisema kuwa mateka huyo angeachiliwa leo jumapili kufuatia maafikiano ya kulipa fidia.
Marekani iliamrisha kuchukuliwa jitihada hizo kwa kuwa iliamini kwamba maisha ya bwana Somers yalikuwa hatarini.
(CHANZO: BBC SWAHILI)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni