Katibu mpya wa CCM wilaya ya Ludewa Lusian Mbosa akisalimiana na Rais Dkt Jakaya Kikwete
Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Bw Mangula akiwa na viongozi wa CCM |
Habari za ndani za chama hicho
kutoka wilaya ya Iringa vijijini na Ludewa zimeeleza kuwa tayari
uongozi wa chama ngazi ya juu umefanya mabadiliko ya makatibu wa
wilaya hizo mbili katika mkoa wa Iringa na Njombe pia mkoani
Katavi na Mbeya na baadhi ya wilaya hapa nchini .
Mbali ya kujipanga kwa uchaguzi mkuu
ila bado habari za ndani zinaonyesha kuwa kuondolewa kwa makatibu
hao katika vituo vyao imetokana na uwezo wao wa kiutendaji pamoja na
kutoelewana na makatibu na mwenyeviti wa CCM ngazi za kata .
Hata hivyo kwa upande wa wilaya ya
Iringa vijijini katibu wake Bi Amina Imbo habari za kuhamishwa
zilivuja mapema mwezi Novemba mwaka huu na kuwa alipaswa
kuhamishiwa Kigoma na nafasi yake Iringa ilidaiwa kuchukuliwa na
Roda George ila baadae suala hilo lilikwama baada ya baadhi ya
viongozi kuingilia kati na kupigania uhamisho huo kusitishwa .
Kutokana na vigogo kuingilia kati
baadhi ya makatibu kata walianza kampeni za chini kwa chini
kupinga katibu huyo kuendelea kuwepo kwa madai kuwa hana ushirikiano
mzuri na wao hivyo ni heri CCM Taifa ilivyoamua kumbadilisha .
Taarifa zilizoufikia mtandao huu wa
matukiodaima leo na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa CCM
zinadai kuwa tayari katibu mpya wa wilaya ya Iringa vijijini
amefika ofisini na kuripoti kwa ajili ya kuanza kazi na kuwa katibu
huyo Mahida Mbogo ametokea wilaya ya Mpanda japo hadi sasa
aliyekuwa katibu wa wilaya hiyo ya Iringa vijijini Amina Imbo
haifahamiki ni wilaya gani atakwenda .
Huku katika wilaya ya Ludewa Eliud
Shemauya habari kutoka kwa makatibu wake wa kata zinadai kuwa
kuhamishwa kwake ni kutokana na kutokuwa mkweli na muwazi katika mambo
yake na hata ushirikiano na makatibu na wenyeviti ulionekana kuwa wa
chini zaidi.
Kwa sasa katibu mpya wa wilaya ya
Ludewa ambae tayari ameripoti ni Bw Luciana Mbosa huku taarifa
zikidai kuwa kuna uwezekano wa katibu huyo kuendelea kuwepo hadi
upite uchaguzi wa serikali za mitaa.
Pia katika wilaya ya Makete tetesi zinadai kuwa katibu wa CCM wilaya hiyo ni miongoni mwa makatibu waliokumbwa na pangua pangua hiyo na chanzo cha kupanguliwa ni kuwa tofauti na mbunge wa jimbo hilo Dr Binilith Mahenge na kumuunga mkono mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Okoka Sanga .
Hizi ndizo tetesi za leo wadau zinafuatiliwa zaidi kupata ukweli wa tetesi hizo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni