UKATILI USIOSEMEKANA DUNIANI,
(Samahani kwa picha mbaya)
Tukio
lilitokea hivi karibuni mkoani Mara la mama wa kambo kumchinja mtoto
wake kwa kutumia panga hadi kufariki, limechukua sura mpya baada ya mama
huyo nae kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kukatwa katwa
na mapanga mpaka kufariki.
Tukio la
kukatwa katwa mapanga mama huyo limetokea baada ya wananchi wa kijijini
hapo walioshikwa na jazba kali kwa kutokubaliana na kitendo cha kinyama
alichomfanyia mtoto huyo kwa kumkatishia maisha yake.
Mwili wa mtoto aliefariki kwa kuchinjwa na mama ake wa kambo kwa kutumia panga linaloonekana hapo chini pichani.
Hata
hivyo wananchi walionekana kujichukulia hatua mikononi kwa kumuua mama
huyo, kwa kile kilichodaiwa hawakuona hatua zozote za kisheria
alizochukuliwa mtuhumuwa huyo kwa kitendo cha kinyama alichokifanya.
Awali
mwenyekiti wa kijiji alifwatwa na wanakijiji kuulizwa ni hatua gani ya
kisheria mtuhumiwa atachukuliwa kwa mauaji ya kinyama aliyoyafanya
kwamaana baada ya tukio, mtuhumiwa alionekana kutochukuliwa hatua yeyote
ya kisheria kwa muda mrefu licha ya serikali ya kijiji na polisi kupata
taarifa ya kutokea tukio hilo. Mwenyekiti wa kijiji aliwajibu
wanakijiji kuwa polisi wanatambua kutokea kwa tukio hilo na watakuja
kumkamata mtuhumiwa na hatua za kisheria za mauaju zote zitafata juu
yake.
Muda
ulizidi kutokomea bila kuonekana dalili zozote za mtuhumiwa huyo
kuchuliwa hatua, ndio wanakijiji wenye hasira kali walipomvamia mama
huyo na kumkatakata kwa mapanga kulipiza kisasi kwa kile alichomfanyia
mtoto wake.
Mwili wa
mwanamke ukiwa umekatwa kwa mapanga na wananchi wenye hasira kali kwa
kitendo alichokifanya cha kumuua mtoto wake wa kambo kwa kumchinja kwa
panga.
Mwenyekiti wa kijiji analilaumu jeshi la polisi kwa kuchelewa kumchukua hatua mtuhumuwa mpaka maafa makubwa mengine kutokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni