Na EmanuelMadafa,Mbeya
Baada ya
kumaliza na kufanikiwa kumrudisha kocha wake, Jumma Mwambusi aliyetishia
kuondoka katika klabu hiyo kutokana na matokeo mabaya, klabu ya Mbeya
City imefanikiwa kumsajili beki kisiki Jumma Nyoso.
Kabla ya kutua Mbeya City, Nyoso alikuwa mchezaji huru baada ya
kumaliza mkataba wake na nyingine ya ligi Kuu ya Coastal Union katika
msimu iliopita .
Kusajiliwa kwa beki huyo kisiki aliyewahi kutamba na timu za Simba na
Taifa stars, huenda ikasaidia kuiokoa timu hiyo na matokeo mabaya
iliyoyapata tangu kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara, Septemba 20
mwaka huu.
Katika michezo saba iliyocheza kabla ya ligi kusimama imefanikiwa
kushinda mchezo mmoja tu na sare michezo miwili, huku ikifungwa michezo
minne.
Hali hiyo ilionekana kuwakera mashabiki wa timu hiyo ambayo msimu
uliopita ilipata mafanikio makubwa na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa
katika nafasi ya tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni