Jumapili, 7 Desemba 2014

WOLPER ATOA MSAADA KWA WAZEE WASIOJIWEZA JIJINI DAR

Jacqueline Wopler (kushoto) akibeba mfuko wa sukari.
Vyakula vilivyotolewa na Jacqueline Wolper katika kituo cha kulelea wazee wasiojiweza
kituo cha  Msimbazi Centre  jijini Dar.
Sister Wilbroda Mangwangi (katikati) na Wolper wakisalimiana.
Wolper akisalimiana na Bibi Rachel Christopher.
Mpishi wa wazee Salma Hamidu.
Wolper akimsalimia mzee ambaye hajiwezi.
Wolper akisaini kitabu cha wageni.
Woper Family.
KATIKA kuadhimisha miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake , msanii wa filamu nchini hapa Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ ametoa msaada  kwa wazee wasiojiweza kituo cha  Msimbazi Centre  jijini Dar, ambacho kiko chini ya kanisa Katoliki.
Kabla ya kutoa msaada huo Wolper alisoma dua nyumbani kwake  na  baadaye kwenda katika kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula kama Mchele kg 100, Unga wa sembe kg 50, sukari  kg 100 na mafuta ya kula madumu mawili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa