"Mheshimiwa Spika,
Kamati imepitia Mkataba wa mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP
na kuthibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Prof.
Sospeter Muhongo (Mb) ndiye alikuwa kiungo kati ya Bw. Harbinder Singh
Sethi wa IPTL na Ndg. Rugemalira wa VIP (Kiambatisho Na. 16). Katika
mkataba huo wa tarehe 19 Agosti, 2013. Ndg. James Rugemalila
alithibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter
Muhongo alimwomba kuwasilisha kiasi cha fedha ambacho angependa kulipwa
na IPTL ili kumaliza Shauri lililokuwepo mahakamani. Aidha, Bw. Sethi
aliwasilisha kwa Bw. Rugemalira ushahidi kwamba PAP imenunua Hisa 7 za
Mechmar katika IPTL. “On 11th July 2013, the Minister of Energy
and Minerals, Hon. Dr. Prof. Sospeter Muhongo invited VIP to submit to
him the amount of money if paid VIP would conclusively settle VIP claims
against IPTL”. Mheshimiwa Spika, mchakato wote wa kutoa
fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW ndipo ulipoanza na mauzo ya hisa
za VIP kwenda PAP na baadaye kuhitimishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya
tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo yaliyotumika kuhalalisha utoaji wa
fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba,
2013" - UKURASA WA 58 WA 'TAARIFA YA KAMATI [YA KUDUMU YA BUNGE
YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)] KUFUATIA MATOKEO YA UKAGUZI MAALUM WA
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KATIKA AKAUNTI YA TEGETA
ESCROW ILIYOKUWA KATIKA BENKI KUU YA TANZANIA'
"Mheshimiwa Spika, Kutokana
na tofauti zilizokuwepo kati ya MECHMAR na VIP kuanzia mwanzo wa mradi,
VIP iliamua kuuza Hisa zake zilizoko IPTL kwa makampuni mbalimbali kwa
nyakati tofauti ikiwemo MECHMAR kama mwanahisa mwenzake, NSSF, Camel
Oil, Great White Shark Opportunity Fund pamoja na SYMBION lakini
haikuwezekana kutokana na kutoafikiana katika bei. Mheshimiwa Spika, Baadaye
VIP chini ya usuluhishi ya RITA, iliuza Hisa zake kwa PAP kwa thamani
ya Dola za Marekani milioni sabini na tano (US$ 75,000,000/=). Ununuzi
wa Hisa Asilimia 30 za VIP uliofanywa na PAP ndiyo uliyomaliza mgogoro
wa Wanahisa uliyokuwa Mahakamani na kuufanya Mtambo wa IPTL kumilikiwa
na PAP kwa kuwa ndiyo iliyomiliki Hisa zote Asilimia 100 za IPTL. Taarifa ya PAC: Katika ukurasa wa 58 wa Taarifa ya PAC imeelezwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye aliyekuwa Dalali Mkuu aliyewakutanisha Bw Harbinder Sethi na Bw James Rugemalira Ufafanuzi Mheshimiwa
Spika, Taarifa hii siyo sahihi kwa kuwa tangu tarehe 9 Novemba, 2011,
RITA aliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL. Wakati huo,
Waziri wa Nishati na Madini aliyeko sasa alikuwa bado hajateuliwa kwenye
wadhifa huo" - UKURASA WA 11-12 WA 'UTETEZI WA SERIKALI' KUPITIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
"Tarehe
15 Agosti 2013 kampuni ya VIP iliingia makubaliano na PAP ya kuuza hisa
tatu (3) katika IPTL, ambapo utekelezaji wa makubaliano hayo ulianza
rasmi tarehe 19 Agosti 2013 kulingana na Kipengele Na. 1.26 cha
Makubaliano ya Uuzaji na Ununuzi wa Hisa hizo (Kielelezo 65 ). Wakati wa
makubalino hayo yanafanyika kampuni ya IPTL ilikuwa katika ufilisi.
Mahakama Kuu ya Tanzania iliridhia (taking judicial notice) makubaliano
haya katika hukumu ya tarehe 5 Septemba 2013" - UKURASA WA 29 WA
'TAARIFA YA UKAGUZI MAALUM [WA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA
SERIKALI (CAG) KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA KAUNTI YA
'ESCROW' YA TEGETA, PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL ILIYOWASILISHWA
NA CAG KWA KATIBU WA BUNGE.'
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni