Makongoro Oging’ na Shani Ramadhan
Msaidizi
wa kazi za ndani (hausigeli), Rehema Ally (17), mkazi wa Yombo,
Machimbo Mwisho, Ilala jijini Dar, amechanwachanwa kwa wembe na kisu
sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyosababisha alazwe katika
Hospitali ya Amana kwa matibabu.
Akizungumza
na Uwazi nyumbani kwa mwajiri wake aliyejulikana kwa jina moja la
Ghati, Yombo jijini Dar, Rehema aliyefika jijini hapa Januari, 2013
akitokea nyumbani kwao, Masasi mkoani Mtwara, alikuwa na haya ya
kusema:
“Nakumbuka
siku hiyo ilikuwa ni Jumapili ya Novemba 30, saa moja usiku nikiwa nje
ya nyumba ya bosi wangu. Akatokea msichana mmoja aitwaye Fatuma na
mwenzake aitwaye Ashura huku wakiwa wamebeba kisu na wembe. Wakanikamata
kwa nguvu na kunikaba, wakaniangusha chini na kuanza kunichanachana
mwili mzima.
“Wakati
huo nilikuwa naelekea nyumbani kwa akina Fatuma kuchukua sanduku langu
ambalo alilichukua kwa bosi wangu akidai kwamba nimempotezea ‘memori
kadi’ ya simu yake hivyo alisema kwamba mpaka nitakapomrudishia ndipo
nitakapochukua sanduku langu.Rehema Ally akionyesha moja ya jeraha alilopata mkononi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni