Ndege ya mizigo iliyosheheni silaha za kivita imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kano nchini Nigeria.
Licha ya
kukanusha awali, Urusi imesema inamiliki ndege ya mizigo iliyozuiwa
katika uwanja wa ndege wa Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya
kugunduliwa imebeba silaha ambazo hazikuwa zimearifiwa.
Hata hivyo,
Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Nigeria, ambaye aliliambia Shirika la
Habari la Urusi TASS kwamba wanamiliki ndege hiyo, amesema silaha hizo
ni za kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa BBC ndege hiyo bado inashikiliwa uwanjani hapo.
Awali, msemaji
wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya
kati aliiambia BBC kwamba hawafahamu chochote kuhusu helikopta mbili,
magari ya kijeshi na silaha nyingine zilizokuwa katika ndege hiyo.
Hata hivyo
baadaye alipiga simu kufuta usemo wake kwa kusema kuwa ndege hiyo
ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya wanajeshi wao, walioko katika kambi
ya N’damena, ambazo zitapelekwa baadaye Ufaransa.
Msemaji wa
Ubalozi wa Urusi mjini Abuja alisema pia ndege hiyo ni yao. Akitatanisha
taarifa aliyoitoa awali kwamba ndege hiyo si yao.
Kwa nini
Ufaransa inatumia ndege ya Urusi kubeba silaha zake? na kwa nini
ilisimama katika uwanja wa Kano, wakati ikiwa inaelekea nchi jirani ya
Chad na hata Cameroun ikitokea Afrika ya kati? Kwanini baadhi ya silaha
hazikuorodheshwa katika ndege hiyo kama zimebebwa?.
Hayo ni maswali yalioulizwa pande zote.
Seriakli ya Nigeria ambayo ndio muhusika mkuu wa tukio hilo, haijasema chochote.
Baadhi ya
wachambuzi wanasema Nigeria inamiliki silaha hizo ilizonunua katika soko
haramu. Wengine wanasema silaha hizo zilinunuliwa kutoka kwa waasi wa
Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wakielezea kwanini ndege hiyo
imeingia nchini humo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Nigeria
imewekewa vikwazo vya silaha kutoka Marekani na nchi hiyo imekuwa
ikiarifiwa kutumia njia zisizo halali kupata silaha kwa ajili ya
kupambana na wapiganaji wa Boko haram.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni