Jumatatu, 22 Desemba 2014

BREAKING NEWS:: WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAKAZI, ANNA TIBAIJUKA AMETENGULIWA RASMI NAFASI YAKE YA UWAZIRI, PROF MUHONGO AWEKWA KIPORO


001

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amemaliza hutuba yake na Wazee wa Jiji la Dar es salaam na Kumalizia kwa Kumuwajibisha waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka kwa kutengua wadhifa wake wa UWAZIRI.mh rais alisema "Waziri Tibaijuka alifanya makosa kimaadili; tumemwomba AnnaTibaijuka apumzike tumteue mwingine!"
Pia Mh Rais amesema kuwa "Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo huyu nimemuweka kwanza kiporo maana bado uchunguzi unafanyika"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa