Simon Sserunkuma akisaini fomu za Simba
Timu ya Simba imekatisha mkataba na wachezaji wake wawili wakimataifa
wote raia wa Burundi, ambao ni Mshambuliaji Hamis Tambwe na Kiungo
Pierre Kwizera ikiwa ni siku moja tangu Simba kuifunga Yanga kwenye
mchezo wa nani mtani Jembe.
Simba Sports Club imetengua ndoa yake na wachezaji hao wawili wote
raia wa Burundi, ili ipate nafasi ya kuwasajili wachezaji wengine wawili
wote raia wa Uganda yaani Mshambuliaji Saimon Sserunkuma, na beki Juuko
Murushid, na zoezi la kuwasajili limefanikiwa leo.
Beki Juuko Murushid akisaini mkataba wa kuichezea Simba…
Wachezaji hao Saimon maarufu kama Sam Sserunkuma na Juuko Murushid,
waliichezea Simba dhidi ya Yanga jana katika uwanja wa Taifa Jijini
Dar-es-salaam, na wote walionesha uwezo mkubwa na kuisaidia Simba kupata
ushindi huo wa mabao mawili dhidi ya Yanga.
Baada ya usajili huu sasa wachezaji wakigeni kutoka Uganda wanafikia
watano katika klabu hiyo, wakiongozwa na beki George Owino, mshambuliaji
Emanuel Okwi, Dan Sserunkuma, Saimon Sserunkuma na Juuko Murushid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni