Ijumaa, 5 Desemba 2014

MSUSI WA HK SALOON AFIA GUEST HOUSE,KIFO CHAKE CHAGUBIKWA NA UTATA


Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume mmoja ambaye ni Msusi katika moja ya Saloon za
wanawake hapa manispa ya Tabora inayofahamika kama HK,Mwanaume huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ramadhani amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la SALAMA GUEST ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu na hatimaye kufikwa na umauti.

Mwili ukichukuliwa na Polisi  baada ya kuvunjwa mlango wa chumba katika  Guest House hiyo.

Dada huyu inasemekana kuwa ndiye alikuwa mpenzi wake marehemu huyo Ramadhani

Baadhi ya wananchi waliofika katika Guest house hiyo kushuhudia tukio hilo.



Hii ndio HK Saloon aliyokuwa akifanyia kazi msusi huyo maarufu wa nywele za akinamama ambapo kifo chake kimegubikwa na wimbi la utata kutokana na maelezo kuwa aliondoka Saloon hapo baada ya kufunga milango na kuelekea huko Guest house akiwa mzima wa afya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa