Floyd Mayweather amethibitisha pambano lake na Manny Pacquiao litafanyika mwaka 2015
HATIMAYE bondia Floyd Mayweather Jnr ametaja Mei 2 mwakani kuwa tare he ya pambano lake na Manny Pacquiao.Tetesi
juu ya ujio wa poambano hilo la utajiri mkubwa zimezidi kuenea tangu
Pacman aonyeshe kiwango kizuri wakati anampiga Chris Algieri mjini
Macau, China wiki mbili zilizopita.Sasa
Mayweather, anazipa kazi ya ziada moja ya kampuni zake promosheni ya
matukio kwa kusema: "Nitapigana na Pacquiao? Sahihi,".
Pacquiao (kulia) alimtaka Mayweather wapambane baada ya kumpiga Chris Algieri mwezi Novemba
Alipoulizwa
litakuwa pambano lake lijalo, akajibu; "Sahihi," na alipotakiwa kutaja
tarehe ya pambano lake lijalo, akasema; "Mei 2, sahihi,".
Bondia
huyo ambaye hajapoteza pambano na anayesifiwa kwamba ndiye mkali wa
kurupa makonde duniani ameongeza; "Watu wanalitaka hikli pambano.
Nalitaka. Kikwazo pekee kilikuwa Bob Arum (promota wa Pacquiao) lakini
nafikiri mabondia wote wanalitaka. Hivyo ni wakati wa
kupambana,"amesema.
13
Dec
2014
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni