Jumapili, 7 Desemba 2014

MAANDALIZI YA SIKU YA UHURU YAPAMBA MOTO

WANATISHA

Majeshi ya ulinzi na usalama yakitoa salamu katika mazoezi.
Vijana wa halaiki wakionyesha ufundi wao.
Vikundi mbalimbali vya ngoma, kwaya na ‘brass band’ vikionyesha sanaa yao.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mazoezi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani)
MAANDALIZI ya siku ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) Desemba 9,  kutimiza miaka 53, yanaendelea  Uwanja wa Uhuru ambapo kutakuwa na gwaride la kijeshi  vikundi vya sanaa, kwaya, halaiki ya vijana, ‘brass band’ na  matarumbeta.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema milango katika Uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi  ambapo wananchi watakaofika katika hafla hiyo watatumia mlango wa kusini upande wa Barabara ya Mandela kuingia uwanjani, na waalikwa wenye kadi watatumoa mlango wa geti namba mbili 2 na viongozi watatumia geti namba tatu 3.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa