Msanii
wa muziki wa Injili, Bonny Mwaitege (kulia) akisalimia na Mtangazaji
wa Radio Kasibante Mwl. Joyce Ruboz mapema leo katika kipindi cha
Gospal Flava cha Kasibante FM 88.5.
Mtumishi
wa Mungu na muimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando akiwa kwenye
studio za radio Kasibante FM 88.5 akionekana mwingi wa furaha wakati
akihojiwa na mtangazaji (hayupo pichani) wa kipindi cha Gospal Flava
leo Bukoba mjini.
Mtangazaji
wa kipindi cha Gospal Flava Mwl. Joyce Ruboz akifurahia jambo baada ya
kuwaona waimbaji wa Injili wakiporomosha sauti zao tamu wakati wa
kipindi chake leo asubuhi.
Mwalimu
Joyce Ruboz pia ni mmoja wa waratibu wa fainali za Biblia mjini Bukoba
katika suala zima la kutanua na kuendeleza jamii kupitia vipindi vya
dini. Wasanii Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula walitinga
ndani ya Radio Kasibante FM tayari kupamba fainali za mashindano hayo
leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 8 mchana.
Boniface
Mwaitege (kulia) akiwa na msanii mwenzake wa Nyimbo za Njili, Gaston
Sapula kwenye Studio za Radio Kasibante FM Bukoba leo.
Mtangazaji wa Radio Kasibante FM 88.5, Abera naye alikuwepo katika Ofisi zao, anapokea wageni kwa tabasamu (hawapo pichani).
Picha ya pamoja Mwalimu Joyce Ruboz na Wasanii wa Injili wanaotarajia kupamba fainali za Biblia leo katika Uwanja wa Kaitaba.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe (wa tatu toka kulia) naye alipata picha ya pamoja na wasanii hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni