Jumatano, 17 Desemba 2014

AKUTWA AMEKUFA SHAMBANI KWAKE







Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yona Mwinuka (52)amekutwa amefaliki katika kibanda ambacho kiko shambani kwake hali ambayo imezua wasiwasi kwa baadhi ya wakulima wanaofanya kazi za kilimo huku wakiishi katika vibanda huko mashambani.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani amesibitisha kutokea tukio hilo amesema mpaka sasa hakuna kinachofahamika chanzo cha kifo chake kutokana na mwili wake kuharibiwa vibaya na Mbwa.

Kamanda Ngonyani alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kifo hicho na baada ya uchunguzi taarifa kamili itatolewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa