Ijumaa, 5 Desemba 2014

UKAWA WAMNADI MGOMBEA WA UWENYEKITI WA KIJIJI LUDEWA MJINI


 Mheshimiwa Diwani Kata ya Mlangali Mr. Faraja Mlelwa (Chadema) akizungumza na wananchi katika viwanja vya soko Ludewa
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini

  Wananchi  wakiwa katika mkutano huo
Mr. Alfreld Chale (kulia) akimsikiliza Diwani akiwa akimnadi kwa wananchi

  Baadhi  ya viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria kampeni hicho.


 
Kampeni hizo zilifanyika katika viwanja vya Soko Katika Kijiji cha Ludewa Mjini jana tarehe 4/11/2014 wakati wa kumnadi Mr. Alfreld Chale anaye gombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji hicho kwa tiketi ya Chadema. 

Katika mkutano huo walikuwepo Viongozi wa vyama vingine vya siasa ikiwa ni pamoja na DP, na Cuf. Wananchi walifurahishwa sana na kumuunga mkono mgombea huyo na kuahidi kuwa hawataweza kumwangusha katika uchaguzi utakaofanyika hapo tarehe 14/12/2014. 

Aidha Mh. Diwani wa Kata ya Mlangali Mr. Faraja Mlelwa aliwaasa wananchi wa Kijiji hicho kufanya mabadiliko ili kuleta maendeleo ya Kijiji hicho na Taifa kwa ujumla.

Pia Mh. Diwani alimpongeza sana Mh. Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kwa ujasiri mwingi hasa kwaajili ya kutetea maslahi ya wananchi wa Ludewa na Taifa kwa ujumla, hivyo aliwaomba tena wananchi kufanya maamuzi magumu katika uchaguzi huo ili kumuunga mkono Mbunge kwa kuweka viongozi makini na wenye nguvu ili kuliponya Taifa letu. Miongoni  wananchi waliohudhuria mkutano huo walikualiana na mawazo ya Diwani huyo pamoja na Mgombea Mr. Alfreld Chale.

Endelea kufuatilia ili kujua nini kinaendelea katika kampeni hizi mhimbilikwetu.blogspots.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa