Ijumaa, 5 Desemba 2014

AJALI BASI LA KAMPUNI YA LUWINZO KITONGA MCHANA WA LEO


                                                    RPC Mungi

MZIMU   wa ajali   waanza  kutesa  mkoani  Iringa baada ya ajali  nyingine  mbaya  kutokea katika mlima wa  Kitonga katika  wilaya ya  Kilolo kwenye barabara  kuu ya Iringa - Dar es Salaam  baada ya  basi la kampuni  ya Luwinzo kunusurika kugongana uso  kwa  uso  na  Lori  kabla ya basi hilo  kupinduka katika  mlima  huo  Kitonga.

Mashuhuda   wa ajali  hiyo  waliozungumza na mtandao huu  wa  www.matukiodaima.co.tz  kwa njia ya  simu  wamedai kuwa ajali  hiyo  imetokea mchana wa  leo  mida ya saa 7 wakati    likitokea   Njombe kwenda jijini Dar es Salaam  .

Shuhuda   huyo  alisema  kuwa dereva  wa basi hilo la Luwinzo aliyekuwa akishuka mteremko  breck zilifeli na  hivyo  kugongana uso kwa  uso na lori ambalo  lilikuwa  likipanda mlima na  kuwa  dereva wa basio hilo  hadi  sasa ni mahututi  huku abiria  wengine  wakijeruhiwa  vibaya.


Wamedai kuwa katika  ajali  hiyo  abiria  zaidi ya 10   wamejeruhiwa na  kuwa hadi  sasa  jitihada za  kuwaokoa majeruhi  hao  zinaendelea kufanywa na   bado polisi  kufika eneo  la  tukio .


Kamanda  wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa Ramadhani Mungi  amethibitisha  kutokea kwa ajali  hiyo na  kuwa  chanzo   cha ajali  hiyo  ni uzembe wa dereva wa basi la Luwinzo  ambae  alikuwa akitaka  kulipita  lori  lenye  tela lililokuwa  mbele  yake.

Kamanda  Mungi  alisema  kuwa  basi hilo  lenye namba  za usajili T 823 DLF  lilitaka  kulipita  lori lenye namba  za  usajili T 691 CDK lenye tena namba T 810 CFJ   na baada ya  kulipita  mbele  lori  lenye namba  za usajili T 865 CYL lenye  tela namba  T 521 CNA  lilikuwa  likija  mbele  hivyo bila dereva  huyo wa basi  kulikwepa lori  hilo ilikuwa  wagongane  uso kwa  uso.

" Baada ya dereva wa basi  kulikwepa  Lori  hilo  ndipo ajali  hiyo  ilipotokea kwa basi  hilo kuanguka na  katika ajali  hiyo uzembe ni  wa  dereva wa basi"

Hii  ni  ajali  ya  pili   kutokea mkoani  Iringa   ndani  ya  siku  tatu wakati  ajali ya  kwanza  ilihusisha  magari  matatu  likiwemo basi la kampuni ya Another G   na kusababisha  kifo cha mtu  mmoja na  28   kujeruhiwa  vibaya ajali  iliyotokea  eneo la Kisolanga Ifunda barabara ya  Iringa - Mbeya .

                        picha  za ajali  hii  utazipata  hapa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa