Alhamisi, 4 Desemba 2014

AJALI

Tuesday, December 2, 2014

AJALI YATOKEA JIONI HII ENEO LA LUGALO IRINGA

Ni majira ya jana jion


Wananchi   wakitazama ajali ya daladala iliyotokea  eneo la Lugalo  mjini Iringa katika barabara ya Iringa - Dodoma  leo
Hili ndilo  gari  lililogongwa na daladala  hilo kabla ya  kupinduka
Wananchi  Iringa  wakishuhudia ajali  hiyo iliyotokea  jioni hii
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
ABIRIA zaidi ya 20 waliokuwa wakisafiri na daladala lenye namba za usajili T475 ACD linalofanya safari zake kati ya stendi ya miyomboni mjini Iringa na Mkimbizi kugongana na gari jingine lenye namba T 491 ABY Toyota kabla ya kupinduka . 

Ajali hiyo imetokea eneo la Lugalo katika barabara kuu ya Iringa - Dodoma wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha majira ya saa 11 jioni hii wakati daladala hilo likitoka mjini Iringa kuelekea Mkimbizi .

 Mashuhua wa ajali hiyo waliozungumza na mtandao huu wa matukiodaima wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa daladala ambae alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake.


 Hata hivyo alisema kuwa eneo hilo ambalo lina tuta kubwa hii ni ajali ya pili kutokea kwa kipindi cha wiki moja na ni ajali ya nne toka ujenzi huo wa barabara uanze. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha zaidi ya baadhi ya abiria zaidi ya wanne kupata majeraha kiasi .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa